Justin Bieber Ajiunga Na Kanye West Kuhudhuria Ibada Jumapili

Nyota wa muziki wa Pop, Justin Bieber amefanya kumshtukiza KanyeWest kwa kwenda kuungana nae kwenye huduma ya kiroho Sunday Service Jumapili ya Jana huko LA nchini Marekani.

Sunday Service ni huduma ya kiroho ambayo huongozwa na msanii Kanye West ambapo mastaa mbalimbali wamekua wakialikwa katika huduma hiyo ambayo hubadilisha nyimbo za kidunia kuwa nyimbo za kumsifu Mungu.
Justin Bieber alihudhuria hafla hiyo ya kusifu na kuabudu kupitia wimbo ambao alipewa nafasi ya kuuimba na akafanya hivyo akipiga Acappella ambayo watu wote waliyokua mahali hapo waliikubali na kumshangilia.


EmoticonEmoticon