Juventus Kuwatoa Wachezaji Wawili Ili Kumpata Pogba, Bei Yake Yawatoa Jasho

Paul Pogba
Juventus inapanga kuwatoa mshambuliaji wa Wales Aaron Ramsey, 29, na wa Ufaransa Adrien Rabiot, 24, kwa Manchester United kama sehemu ya kitita cha £125m ili kujaribu kumrejesha mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba 26.
Ajenti wa Pogba, Mino Raiola, amesema kwamba alifanya mazungumzo na Juventus kuhusu mchezaji huyo na kuna uwezekano wa kuondoka Manchester United msimu ujao.
Manchester United inataka kumuuza Pogba kwa £100m kabla ya michuano ya Euro 2020 ili kupata pesa za kufikia wanaowalenga dirisha la usajili litakapofunguliwa.


EmoticonEmoticon