Kauli Za Raisi Donald Trump Baada Ya Kushinda Kesi Iliyokuwa Inamkabili

Donald Trump Akifurahia
Rais wa Marekani Donald Trump amefurahia ushindi baada ya kuondolewa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili, ndani ya Ikulu ya Marekani amewaponda wapinzani wake wa kisiasa.
''Nimefanya makosa kwenye maisha yangu, nitakiri......lakini haya ndio matokeo, '' alisema huku akinyanyua gazeti lililokuwa na kichwa cha habari ''Trump hana hatia''.
''Tumepita kubaya, hatukutendewa haki.Hatukufanya kosa lolote,'' alisema Ikulu. ''Ulikuwa uovu, ilikuwa rushwa.''
'' Sasa tuna neno zuri. Sikufikiria kama litakuwa zuri namna hii, ''Linaitwa kusafishwa kabisa.''
Trump akiwa ameshika Gazeti Lililotoa Habari za Ushindi wake
Trump alishtakiwa na bunge la wawakilishi mwezi Desemba kwa matumizi mabaya ya madaraka na kulizuia Bunge kutekeleza majukumu yake, lakini hakukutwa na hatia siku ya Jumatano baada ya mchakato wa majuma mawili wa kesi dhidi yake kwenye bunge la seneti linalodhibitiwa na chama cha republican.
Trump pia alieleza kuhusu uchunguzi uliokuwa ukifanyika kuhusu kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016 na uhusiano na Kremlin.
''Ulikuwa upumbavu mtupu,'' alisema '' Hili suala halipaswi kutokea tena kwa rais atakayefuata.''
Trump alisema kuwa bado ana imani na chama cha Republican wakati huu wakielekea kwenye uchaguzi ujao wa mwezi Novemba.
Trump akiwa ameshika Gazeti Lililotoa Habari za Ushindi wake
Sherehe baada ya kusafishwa kwake kulitofautiana na rais Bill Clinton ambaye alihutubia mwaka 1999, alipoomba radhi kwa raia wa Marekani, baada ya kushtakiwa.
''Ninataka kusema tena kwa raia wa Marekani ninaomba radhi kwa kile nilichokisema na kwa mzigo mkubwa walioubeba wabunge na raia wa Marekani kwa ujumla,'' Bwana Clinton alieleza.
Alipokuwa akimaliza kuzungumza, Trump aliomba radhi kwa familia yake, kwa ''kupita kwenye misukosuko hiyo''.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon