Kocha Wa Liverpool Klopp Arudisha Barua Ya Majibu Kwa Kijana Wa Miaka 10 Ambayo Amekataa Maombi Ya Mtoto Huyo


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameandika barua ya kumjibu shabiki mtoto wa Man United Daragh mwenye umri wa miaka 10 ambaye aliandika na kueleza hisia zake kuhusiana na ubora wa Liverpool kwa sasa inayoonekana kushinda karibia kila mchezo.

Daragh ameandika barua hiyo na kumuomba Klopp kuwa haruhusu Liverpool ifungwe hata mchezo mmoja kwani wakiendelea kushinda kila mechi na wakashinda kwa mechi 9 mfululizo wataandika historia ya kipekee ambayo Daragh kama shabiki wa Man United itamuuzi sana.
Klopp alijibu barua hiyo na kumshukuru kijana Daragh kwa kutuma ujumbe huo lakini alieleza msimamo wake kuwa hilo haliwezi kutokea, yeye kuruhusu timu yake ipoteze.EmoticonEmoticon