Maamuzi Ya Papa Francis Kuhusiana Na Wanaume Waliooa Kuwa Mapadre

Papa Francis
Papa Francis amepinga kura ya kuwatawaza wanaume waliooa katika jimbo la Amazon kama njia ya kutatua tatizo la uhaba wa makasisi wa Kikatoliki.
Maaskofu waliunga mkono hatua hiyo mwaka jana, lakini uamuzi huo ulihitaji idhini ya Papa kutekelezwa.
Makasisi wa Kikatoliki wanatakiwa kuheshimu sheria ya useja isipokua katika baadhi ya matukio ya ambapo wachungaji wa Kianglikana waliooa walipojiunga na ukatoliki na kukubaliwa kuwa mapadre.
Useja huonekana kwa mtu kama njia ya kujitolea maisha yake kwa Mungu.
Taarifa kutoka Vatcan ilisema: "Amazon inatutia Changamoto, Papa aliandika, kuyashinda matatizo makubwa nana sio kuridhishwa na suluhu ambazo zinatatua sehemu tu ya hali."
Papa alisema kuwa kuna haja kwa makasisi wanaonaoelewa hali ya Amazon na tamaduni zake kutoka ndani ya kanisa. Tunahitaji maaskofu "kuboresha sala kwa ajili ya kuombea wito wa upadre" na kuwatia moyo wale wanaotaka kuwa wamishonari "kuchagua kufanyia kazi yao katika kanda ya Amazon".
Papa Francis
Mwezi Oktoba mwaka jana, kongamano la maaskofu wa kikatoliki(synod ya 184) ilikutana kujadili hali ya baadae ya kanisa hilo katika jimbo la Amazon. Ilidaiwa kuwa wanaume wakongwe waliooa wanapaswa kuruhusiwa kuwa mapadre.
Hata hivyo, wanahitaji kuwa wanaume ambao wanaheshimika na zaidi watoke katika jamii za wazawa ambako wanaazimia kufanyia kazi.
Inakadiriwa kuwa takriban 85% ya vijiji katika Amazon hawawezi kufanya ibada kila wiki kutokana na ukosefu wa mabadre. Baadhi wanasemekana kuwa humuona padri mara moja kwa mwaka.
Lakini vuguvugu lenye itikadi kali za Kanisa Katoliki - hususan katika bara la Ulaya na Marekani - limezungumza kupinga wazo hilo, likidaikwamba hii inaweza kusababisha kukomeshwa kwa useja duniani.
Papa Francis awali alisema kuwa ataangalia uwezekano wa viri probati (yaani wanaume wenye imani iliyodhihirika) kufanya baadhi ya majukumu.
"Tunapaswa kufikiria ikiwa kuna uwezekano wa viri probati ," aliliambia gazeti la Ujerumani la Der Zeit.
Pia Jumatano, Papa a;itangaza kuwa ameamua kutowaruhusu wanawake kuhudumu kama viongozi wa kanisa kwa cheo cha ushemas, ambacho mtu hupewa kabla ya kutawazwa kuwa padre.
Kando na hilo alitoa wito wa kulindwa kwa mazingira katika jimbo la Amazon kutokana na umuhimu wake katika kuzuwia ongezeko la joto duniani.
"Tunadai mwisho wa kuendewa vibaya na kuharibiwa kwa mama dunia ,"alisema Papa Francis.
credit:bbc


EmoticonEmoticon