Maboresho Ya DM Ndani Ya Mtandao Wa Instagram, Taarifa Muhimu Mpya Ikufikie

Mtandao wa instagram
Sehemu hiyo mpya itakuwa ndani ya ukurasa wa DM ambapo chini ya meseji uliyo tumiwa utaweza kuona sehemu mpya ya emoji za reaction ambazo zinafanana kabisa na zile zilizopo kwenye sehemu ya Facebook comment.


via GIPHY


Kama unavyoweza kuona hapo juu, hivyo ndivyo itakavyokuwa kwenye ukurasa wa DM ambao sasa utaweza kujibu meseji ya mtu kwa kutumia reaction. Hata hivyo kwa mujibu wa Jane Manchun Wong @wongmjane ambaye ndiye aliyegundua sehemu hiyo kabla ya kutoka kwake, ameandika kwenye twitter kuwa sehemu hiyo inatarajia kuja hivi karibuni kwani meneja wa mawasiliano na teknolojia aliyemtaja kwa jina la @alexvoica ame thibitisha kuwa sehemu hiyo ipo kwenye majaribio.
DM Reaction Instagram
Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi za lini sehemu hii itawafikia watumiaji wote. Hadi sasa inasemekana sehemu hii ipo kwenye hatua za awali za majaribio na bado haijafika kwenye programu za majaribio za Instagram.


EmoticonEmoticon