Manchester City Yapigwa Marufuku Kushiriki Katika Ligi Ya Mabingwa

Manchester City imepigwa marufuku kushiriki katika ligi ya mabigwa Ulaya kwa misimu miwili ijayo baada ya kupatikana kwamba wamekiuka sheria za Uefa zinazoambatana na masuala ya fedha na leseni.
Mabingwa hao wa ligi ya Premier pia wamepigwa faini ya euros milioni 30 (£25m).
Hata hivyo umauzi huo unaweza kupigwa katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo.
Manchester City imesema kwamba hatua hiyo ni jambo la kukatisha tamaa lakini wala halikuwashangaza na watakata rufaa.
Bod ya udhibiti wa masuala ya fedha imesema City imevunja sheria kwa kuweka kiwango cha juu zaidi cha fedha katika mapato yake ya ufadhili kwenye mahesabu yake na katika ripoti ya fedha iliyowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 ilionesha kwamba hawakupata hasara wala faida", na kuongeza kwamba klabu hiyo haikutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi".
Imesemekana kwamba City huenda pia ikapunguziwa pointi katika ligi ya Premier kwasababu sheria ya udhibiti wa masuala ya fedha katika ligi ya Premier kwa kiasi kikubwa inafanana na Uefa japo hazifanani moja kwa moja.
Hata hivyo, adhabu hiyo haitakuwa na athari zozote kwa timu ya wanawake ya City.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Manchester City: "Klabu hiyo imekuwa ikifikiria umuhimu wa kuwa na bodi huru na kufuatwa kwa mchakato usiopendelea upande wowote kuangalia ushahidi wao ulio wazi.
"Desemba 2018, mchunguzi mkuu wa Uefa alisema wazi vikwazo ambavyo anataka City iwekewe hata kabla ya uchunguzi kuanza kufanywa.
"Kasoro na udhaifu uliopo katika mchakato wa Uefa kwenye uchunguzi alioongoza, hakukuwa na shaka na matokeo ya uchunguzi huu. Klabu hii awali ilikuwa imewasilisha malalamiko yake kwa bodi ya nidhamu ya Uefa, ambayo yaliidhinishwa na mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo.
"kwa maneno rahisi, hii ni kesi iliyowasilishwa na Uefa, ikashtakiwa na Uefa na aliyetoa uamuzi ni Uefa. Kwa mchakato wa kibaguzi aina hii ambao umemalizika, klabu hii sasa itatafuta hukumu isiyopendelea upande wowote haraka iwezekanavyo na hivyo basi, kwanza kabisa itaendelea na mchakato wake katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo bila kuchelewa."
City imepangwa kucheza na Real Madrid katika timu 16 za mchujo za ligi ya mabingwa huku mchuano wa kwanza ukiwa ni Februari 16 katika uwanja wa Bernabeu.
Rais wa La Liga Javier Tebas iliisifu Uefa kwa kuchukua hatua stahiki.
"Kuhakikisha utekelezaji wa sheria ya udhibiti wa fedha na kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria hiyo ni jambo la msingi kwa hatma ya mpira wa kandanda," amesema.
"kwa miaka mingi tumekuwa tukitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua muafaka dhidi ya Manchester City na Paris Saint-Germain, na hatimaye tumepata mfano bora na ni matumaini yetu kwamba hili litaendelezwa. Ni kheri kuchelewa kuliko kutochukuliwa kwa hatua kabisa."


EmoticonEmoticon