Maneno Ya Ole Gunna Baada Ya Kumsajili Odion Ighalo Wa Nigeria

Odion Ighalo
Manchester United imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Watford Odion Ighalo kutoka Shanghai Shenhua kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.
Makubaliano ya kumsajili mchezaji wa kimataifa Ighalo, 30, Old Trafford inakuwa haina chaguo jengine zaidi ya kumnunua.
Ighalo, ambaye bado yuko China anatarajiwa kusafiri kwenda Uingereza ndani ya siku chache zijazo, alifunga mabao 39 katika mecho 99 alizocheza Watford kati ya mwaka 2014 na 2017.
"Odion ni mchezaji mwenye tuzoefu mkubwa," amesema mkufunzi wa United Ole Gunnar Solskjaer.
"Ataingia na kuongezea idadi ya washambuliaji tulionao katika kipindi kifupi atakachokuwa nasi.''
"Mchezaji mahiri sana katika kazi yake, atakuwa na manufaa makubwa hapa." alisema Solskjaer.


EmoticonEmoticon