Marufuku Viza Kutolewa Kwa Wasio Na Ujuzi

Wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi hawatapata viza chini ya mpango mpya wa uhamiaji wa serikali baada ya Uingereza kujiondoa katika Muungano wa Ulaya.
Serikali inahamasiha waajiri kuacha kutegemea wafanyakazi wa kulipwa mshahara wa chini kutoka Ulaya na kuwekeza zaidi katika kudumisha wafanyakazi na kuendelezea teknolojia.
Wizara ya mambo ya ndani imesema Ulaya na raia wa nchi ambazo sio wanachama wa Muungano huo watakuwa wanachukuliwa walio katika daraja moja baada ya usafiri huru kati ya Uingereza na Muungano wa Ulaya kufikia ukomo wake Desemba 31.
Makampuni yanasema sheria kali kama hizo zitafanya iwe vigumu kuvutia wafanyakazi.
Lakini waziri wa mambo ya ndani Priti Patel amesema utekelezaji wa mfumo mpya kutamaanisha watu wenye weledi tu ndio watakaoingia Uingereza.
Serikali ambayo ilisema inalenga kupunguza wahamiaji kwa ujumla Uingereza, inataka kuanzisha mfumo wa uhamiaji wa kutumia alama ambazo mtu atakuwa anapata baada ya kutimiza vigezo kama ilivyo ahidi katika manifesto yake wakati wa uchaguzi.
Chini ya mfumo huo, wafanyakazi wa nchi za nje ya Uingereza ambao wangetaka kuingia Uingereza itakuwa lazima wawe na uwezo wa kuzungumza Kiingereza na mtaalam kwa kazi fulani baada ya kuidhinishwa na atakayemdhamini.
Wakati wa mchakato huo mhamiaji atakuwa anapewa alama 50 iwapo atatimiza vigezo hivyo.


EmoticonEmoticon