Mbwana Samatta Awataka Radhi Mashabiki Wa Tanzania Wanaofanya Jambo Hili

Mbwana Samatta
Nahodha wa Taifa Stars anayechezea Klabu ya Aston Villa, Mbwana Samatta ameomba Watanzania kuacha kutoa maneno ya kashfa kwenye akaunti za timu na za wachezaji. Baadhi ya mashabiki toka Tanzania wamekua wakifanya kitendo hicho ambacho amesema hakimfurahishi.

"Mashabiki wa soka Tanzania nafaham kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vzr ktk timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mlengo mbaya katika ac/ za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi,” ameandika Samatta.


EmoticonEmoticon