Mfahamu Binadamu Mwenye Uwezo Wa Kusoma Kurasa Ya Kitabu Kwa Sekunde 3

Anne Jones
Anne Jones ana rekodi ya kusoma kwa haraka zaidi Duniani, akiwa na wastani wa kusoma maneno 4,200 kwa dakika ambapo wastani wa kasi ya kawaida kwa Mwanadamu ni maneno 220 hadi 300 kwa dakika.
Mwaka 2007, alifanikiwa kumaliza kusoma kitabu cha Harry Potter chenye jumla ya kurasa 784 kwa muda wa dakika 47.
Hivyo, Anne aliweza kusoma maneno 4,200 kwa dakika, akiwa na wastani wa kusoma kurasa moja kwa sekunde 3.
Kwa kuhakikisha kuwa ameweza kufanya hivyo, aliorodhesha point zote zilizopo kwenye kitabu hicho kwa waandishi wa habari na mwishowe wakaridhia.
Pamoja na kuweka rekodi hiyo, Anne alikuwa akishikilia rekodi ya kuwa Mshindi wa Mashindano ya Dunia ya Kusoma Haraka (World Championship Speed Reading Competition) kwa mara 6.


EmoticonEmoticon