Mizinga 19 Hewani Kwenye Mazishi Ya Hayati Daniel Arap Moi


Rais wa awamu ya pili wa Kenya hayati Daniel arap Moi amezikwa siku ya jumanne feb 13 baada ya jeshi kutoa heshima kwa kupigiwa mizinga 19.
Maafisa wa kijeshi walitoa heshima kwa kufyatua mizinga lilipo kaburi eneo la Kabarak. Ndege za kijeshi ziliruka kutoa heshima kwa hayati Moi.
Tofauti na mtangulizi wake Mzee Kenyatta, ambaye alipata heshima ya mizinga 21, Mzee Moi alipigiwa heshima ya mizinga 19 kwa kuwa alifariki akiwa tayari ameondoka madarakani.
Mizinga ilifyatuliwa kwa mpangilio wa kila dakika tatu.
Moi amezikwa kijijini kwake kaaribu na kaburi la marehemu mkewe Lena aliyeaga dunia mwaka 2004.
Mwili wa rais mstaafu Daniel Moi uliondoka katika chumba cha kuhifadhi mili cha Lee Funeral jijini Nairobi mwendo wa saa moja asubuhi huku msafara wake ukielekea katika uwanja wa ndege wa Wilson ambapo uliwasili nyumbani kwake huko Kabarak muda wa saa mbili na dakika 40.


EmoticonEmoticon