Mtoto Wa Siku Moja Aambukizwa Virusi Vya Corona, Walichokisema Wataalamu

Mtoto mchanga

Mtoto mchanga nchini China ameambukizwa virusi vya corona saa 30 baada ya kuzaliwa, kisa chenye kuhusisha mtoto mchanga zaidi kuwahi kurekodiwa, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Mtoto alizaliwa tarehe 2 mwezi Februari katika hospitali moja ya mjini Wuhan, ulio kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo.
Mama wa mtoto alikutwa na virusi hivyo kabla ya kujifungua. Haijulikani ni kwa namna gani kichanga hicho kiliambukizwa.
Shirika la habari la China, Xinhua limeripoti taarifa za maambukizi siku ya Jumatano.
Ilieleza kuwa mtoto aliyekuwa na uzito kilogramu 3.25, alikuwa na hali nzuri na alikuwa akifanyiwa uchunguzi.
Wataalamu wa afya wanasema inawezekana ni maambukizi yaliyotokea tumboni.
Wataalamu
''Hii inatukumbusha kuwa makini kuwa kuna uwezekano kukawa na maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.'' Daktari wa hospitali ya watoto kitengo cha dawa, Zeng Lingkong aliliambia shirika la habari la Reuters.
Lakini pia inawezekana mtoto aliathirika baada ya kuzaliwa na kuwa karibu na mama yake.
''Inawezekana kuwa mtoto alipata maambukizi kwa njia za kawaida- kwa kuvuta hewa iliyotoka kwa mama alipokohoa,'' daktari wa magonjwa ya maambukizi Stephen Morse ameeleza.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon