Mwanajeshi Aliyewauwa Watu 26 Naye Ameuawa

Mwanajeshi aliyewaua watu 26 kwa bunduki katika mji wa Nakhon Ratchasima,Thai ameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama, kulingana na polisi wa Thai.
Jumamosi, Jakraphanth Thomma alimuua komanda wa polisi na kuiba silaha katika kambi ya jeshi.
Mshukiwa huyo aliendelea kuvamia raia waliokuwa katika shughuli zao barabarani kwenye mji wa kibiashara wa Nakhon Ratchasima, ambao pia unafahamika kama Korat.
Mwanamume huyo ambaye alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wakati anafanya masambulizi, alipigwa risasi baada ya kuzingirwa usiku kucha katika jengo alilokuwemo.
Waziri Mkuu wa Thailand Prayuth Chan-ocha, Jumapili amesema kwamba idadi ya waliouawa ni zaidi ya 20 iliyoripotiwa awali na wengine 57 wamejeruhiwa.
"Hiki ni kisa cha kwanza kutokea Thailand, na nitaka hii iwe mara ya mwisho kisa kama hiki kinatokea," alisema hayo baada ya kutembelea waliojeruhiwa katika hospitali ya Nakhon Ratchasima.
Waziri mkuu ameongeza kwamba nia ya shambulio hilo inasemekana ni kulipiza kisasi baada ya mshambuliaji Jakraphanth kuamini kwamba amelaghaiwa katika makubaliano ya kununua kipande cha ardhi.
Taarifa za awali zimesema kuwa mshambuliaji huyo, 32, halijaribu kutoroka kupitia mlango wa nyuma.
Mama yake mshambuliaji pia aliletwa kwenye eneo la tukio ili kumshawishi mtoto wake ajisalimishe.


Mmoja kati ya waliookolewa aliiambia BBC vile yeye na wenzake walivyojificha chooni ghorofa ya nne kabla ya kutoroka hadi ghorofa ya pili na kujificha chini ya meza moja mgahawani kwa saa tatu, ambapo walisikia karibu milio minne ya risasi kabla ya kuona wanajeshi waliokuja kuwaokoa.

Charlie Crowson, mwalimu anayefunza Kiingereza ambaye anaishi Nakhon Ratchasima, ameiambia BBC miili ya watu waliokufa imetapakaa barabarani katika mji ambao kawaida huwa na Amani.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon