Odion Ighalo Atengwa, Apigwa Marufuku Kujichanganya Na Wenzake

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United, Odion Ighalo amepigwa marufuku kujichanganya na wachezaji wenzake kwenye eneo la mazoezi la klabu hiyo kutoka na hofu ya hatari ya virusi vya Corona baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea nchini China.

Ighalo amejiunga na Manchester United kwa mkopo akitokea klabu ya Shanghai Shenhua ya China hadi mwisho wa msimu huu, amekuwa akifanya mazoezi na Mkurugenzi binafsi katika eneo tofauti na wachezaji wenzake katika viunga vya Manchester.

Nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria amekuwa akifanya mazoezi yake mbali na kiwanja cha mazoezi cha United AON Training Compex kwa kuhofia hali ya kiafya na usalama dhidi ya virusi vya Corona nchini China ambapo mpaka sasa zaidi ya watu 1000 wameripotiwa kufariki dunia huku zaidi ya watu 45, 000 wakiwa tayari wameshaambukizwa na virusi vya Corona.

Ighalo amejiunga na United wiki mbili zilizopita lakini bado hajafanya mazoezi na wachezaji wenzake.


EmoticonEmoticon