Onyo La Raisi Wa Uturuki Kwa Serikali Ya Syria

Raisi wa uturuki
Rais wa Uturuki ameionya serikali ya Syria kwamba italipa gharama kubwa kwa mashambulio dhidi ya wanajeshi wake katika eneo la kaskazini mashariki mwa Syria.
Wanajeshi watano wa Uturuki waliuawa katika mji wa Idlib unaodhibitiwa na upinzani siku ya Jumatatu huku jeshi la Syria likiendelea kusonga mbele katika eneo la vita.
Wanajeshi wa Uturuki walifyatua makombora kadhaa ili kujibu shambulio hilo , lakini rais Recep Tayyip Erdogan alisema: Tutaendelea na mashambulizi.
Wakati huohuo wanajeshi wa Syria walikaribia kuikomboa barabara ya eneo la kaskazini la taifa hilo.
Shirika la haki za kibinadamu lenye makao yake huko Uingereza SOHR liliripoti siku ya Jumanne kwamba wanajeshi wa Syria waliwafurusha waasi na wapiganaji wa kijihad kutoka eneo la mwisho ambalo walikuwa wakidhibiti magharibi mwa mji wa Aleppo.
Hatahivyo hakuna thibitisho kutoka kwa jeshi ama vyombo vya habari vya serikali na kwamba kulikuwa na ghasia katika maeneo kadhaa ya barabara hiyo kuu siku ya Jumanne jioni.
Serikali haijafanikiwa kudhibiti eneo lote la barabara hiyo , ambayo inaunganisha mji wa Aleppo na mji mkuu wa Damscus mbali na mpaka na taifa la Jordan tangu 2012.


EmoticonEmoticon