R Kelly Kupatiwa Dhamana Baada Ya Kukaa Ndani Kwa Miezi Kadhaa

Rkelly
Mwimbaji mkongwe R.Kelly huwenda akapewa dhamana kuhusiana na kesi yake ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo baada ya kukaa miezi kadhaa nyuma ya nondo

Jaji wa mjini Illnois, Harry D. Leinenweber amelikubali ombi la wanasheria wa Kellz juu ya kusikilizwa kwa dhamana ya mteja wao.

Kama R. Kelly akipatiwa dhamana basi atabaki kwenye kifungo cha ndani huku miguu yake ikifungwa kifaa maalum cha kutoa taarifa endapo ana mpango wowote wa kutoroka. Dhamana hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa March 5 mwaka huu.


EmoticonEmoticon