Raia Wa Ufaransa Wapigwa Marufuku Kuwa Wagonjwa

Mameya tisa nchini Ufaransa wamepiga marufuku watu kuwa wagonjwa katika hatua isio ya kawaida kuhamasisha ukosefu wa madaktari.
Makubaliano hayo yaliyotiwa saini na mameya hao wa Sarthe , eneo moja la magharibi mwa Paris, yanasema wagonjwa wanaotafuta matibabu kutokana na ajali ama ugonjwa hawataruhusiwa kufanya hivyo.
Wanasema kwamba lengo lao ni kuionya serikali kuhusu ugumu unaotokana na kupata matibabu katika eneo hilo. Matatizo ya ukosefu wa maafisa wa afya, ukosefu wa vitanda na kufungwa kwa vifaa ni miongoni mwa maswala yalioangaziwa.
Makubaliano hayo yanasema kwamba ni marufuku kutafuta matibabu kupata ajali ama kuzaliwa na tatizo la kiafya katika eneo hilo.
Hatahivyo inaruhusiwa kuelekea mjini Paris kupata matibabu, yameongezea makubaliano hayo. Makubaliano hayo hatahivyo hayajaidhinishwa kisheria . Imetajwa kuwa sheria kali lakini isiyo ya kawaida.
"Tunataka kuiambia serikali kuhusu ukosefu wa madakatari '', alisema Domonique Dhumeaux , rais wa muungano wa mameya wa mashambani na meya wa eneo la Fercé-sur-Sarthe.

''Ni tatizo linalokabili eneo letu. Serikali inafaa kulikabili suala hilo moja kwa moja''.
Bwana Dhumeaux alisema watu 70,000 kati ya 560,000 ambao wanaishi katika eneo hilo hawawezi kupata matibabu. Alisema kwamba hali ya kuwepo mashambani kwa vituo vya matibabu inaongeza hatari kwa wagonjwa.
Dhumeaux aliwataka mameya wengine katika eneo hilo kutia saini makubaliano hayo.
Ukosefu wa matibabu ni suala nyeti katika kiwango cha kitaifa. Mwaka ulioipita utafiti ulibaini kwamba zaidi ya wafaransa wanne kati ya 10 walikuwa wamesalimu amri kuhusu kutafuta matibabu kutokana na kulazimika kusubiri mara kwa mara.


EmoticonEmoticon