Rapa Pop Smoke Afariki Dunia Akiwa Na Umri Wa Miaka 20

Rapa aliyekua akichipukia katika kiwanda cha muziki wa Dunia Pop Smoke amefariki Dunia asubuhi ya leo Jumatano kwa kupigwa risasi na majambazi waliomvamia nyumbani kwake.

Taarifa za awali ambazo zimeripotiwa na TMZ zinasema kuwa rapa huyo mwenye miaka 20, alivamiwa nyumbani kwake maeneo ya Hollywood Hills majira ya saa 10 usiku na wanaume wawili waliokua wamejifunika nyuso zao wakiwa ndani ya makoti yenye kofia zinazofunika kichwa na kumpiga risasi rappa huyo.

Baada ya tukio hilo rapa huyo alichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya Cedar-Sinai Medical Center huko magharibi mwa Hollywood ambapo baadae ilitangazwa kuwa amefariki Dunia.
Pop Smoke anafahamika zaidi kwa wimbo wake wa "Welcome To The Party" ambao aliutoa mwezi April mwaka uliopita, ameshirikiana na wasanii kama vile Travisscott, Quavo, NickMinaj na wengineo kibao.


EmoticonEmoticon