Rasmi Uingereza Yajiondoa Umoja Wa Ulaya

Uingreza hatimaye imejiondoa rasmi kutoka Muungano wa Ulaya baada ya kuwa mwanachama kwa miaka 47 na baada ya miaka zaidi ya mitatu tangu ilipoamua kufanya hivyo katika kura ya maoni.

Hatua hiyo ya kihistoria ambayo ilifanyika saa sita usiku saa za Uingereza iliadhimishwa kwa sherehe na mandamano kwa wale waliopinga hatua ya nhi hiyo kujiondoa Muungano wa Ulaya maarufu kama Brexit.

Mishumaa iliwashwa kuadhimisha siku hiyo huko Scotland, ambayo ilipiga kura ya kubaki EU, huku waliopiga kura kuondoka wakisherehekea Mjini London katika bustani ya bunge.


EmoticonEmoticon