Real Madrid Au Juventus? Pogba Awaambia Wachezaji Wenzake Hili

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amewaambia wachezaji wenzake kuwa anahitaji kuondoka kipindi cha majira ya Joto.

Mfaransa huyo hajaonekana uwanjani tangu mwezi Disemba, huku akiwa ameanza mechi sita pekee msimu huu kutokana na matatizo ya ‘ankle’.

Kwa mujibu wa Manchester Evening News, wachezaji wenzake wanaamini kuwa mawazo ya Pogba kwa sasa hayapo tena ndani ya klabu hiyo huku karibia nyota wote wa United wakimtaka atimke kwa faida ya kikosi.

Hata hivyo inadaiwa kuwa,Pogba bado ni mtu muhimu ndani ya kikosi na hata nje ya miamba hiyo ya soka duniani.

Taarifa kutoka Italia mapema mwezi huu inadaiwa Juventus imedhamiria kumrudisha mchezaji huyo aliyemuuza kwa United  kwa dau la paundi milioni 89 mwaka 2016.

Real Madrid nayo kwa muda mrefu imekuwa ikihitaji kumsajili, Pogba huku ikiwa ikiwa na chaguo la kuwanunua Toni Kroos na Luka Modric.

Baada ya kukipiga dhidi ya Watford Disemba 22, na siku ya Boxing Day mbele ya Newcastle na baada ya hapo, Pogba akaelekea kwenye upasuaji.


EmoticonEmoticon