Somalia Watangaza Hali Ya Dharura Kwa Uvamizi Uliotokea

Somalia imetangaza hali ya dharura kutokana na kuenea kwa kundi kubwa la nzige katika eneo la Afrika Mashariki.
Waziri wa kilimo nchini humo amesema kuwa wadudu hao wameonekana kuwa tishio kwa kuwa tayari wameshambulia mimea mingi ya chakula na kufanya hali ya usalama wa cha chakula Somali kuwa hatarini.
Kuna hofu kuwa hali hii inaweza kushindwa kudhibitiwa kabla ya muda wa mavuno mwezi Aprili.
Umoja wa mataifa umesema kuwa uvamizi wa nzige wengi kiasi hiki haujawahi kutokea Somalia na Ethiopia kwa miaka 25.
Huku nchi jirani ya Kenya, haijawahi kukutana mashambulizi ya nzige kiasi hiki kwa kipindi cha miaka 70 iliyopita, kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa (FAO).
Nzige
Ingawa Somalia imekuwa nchi ya kwanza kutangaza kuwa na hali ya dharura.

Somalia ambayo imekuwa katika changamoto za hali ya kiusalama haiwezi kutumia dawa ya kunyunyizia kwa kutumia ndege ili kuuwa wadudu hao.
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa usaidizi wa kimataifa kukabiliana na nzige wengi waliovamia maeneo ya Afrika mashariki.
Msemaji wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa (FAO), ametoa wito wa kutolewa kwa msaada ili kukabiliana na athari za nzige kama vile ukosefu wa chakula, utapiamlo na kuathirika kwa mfumo wa maisha ya kila siku.


EmoticonEmoticon