Taarifa Za Maziko Na Kuagwa Kwa Mwili Wa Marehemu Rapa Pop Smoke

Taarifa mpya kuhusu marehemu Pope Smoke ni kwamba mwili wake utaagwa na kupewa heshima za mwisho siku ya Jumapili, zoezi ambalo litafanywa na familia na ndugu wa karibu pekee. Umeripoti mtandao wa TMZ.

Itakumbukwa Marehemu Pope Smoke (20) aliuawa wiki iliyopita kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mjini Hollywood Hills kwenye tukio ambalo linatajwa kuwa la kupangwa na sio uvamizi kama ambavyo iliripotiwa awali.

Pop Smoke anafahamika zaidi kwa wimbo wake wa "Welcome To The Party" ambao aliutoa mwezi April mwaka uliopita, ameshirikiana na wasanii kama vile Travisscott, Quavo, NickMinaj na wengineo kibao.


EmoticonEmoticon