The Game Aamua Kumuenzi Marehemu Kobe Bryant Kwa Kuchora Tattoo Usoni Mwake

Mkali wa muziki wa hip hop, Jayceon Taylor maarufu kwa jina la TheGame, mapema wiki hii aliamua kuchora tattoo juu ya jicho kwa ajili ya kumkumbuka nyota wa mchezo wa kikapu Kobe Bryant aliyepoteza maisha.
The Game anaamini Bryant alikuwa mmoja kati ya mastaa wa kikapu duniani, hivyo kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa sana. Kutokana na hali hiyo ameamua kuchora namba 8 ambayo ni jezi aliyokuwa anaitumia katika timu ya Los Angeles Lakes.

Bryant alipoteza maisha kwa ajili ya helikopta, Junuari 26, huku akiwa na mtoto wake wa kike Gianna pamoja na watu wengine saba.

Mbali na The Game kuchora tattoo hiyo, lakini wapo mastaa mbalimbali ambao wamefanya hivyo kama vile rapa 2 Chainz ambaye alichora namba ya jezi kwenye miguu yake yote miwili.


EmoticonEmoticon