Ujumbe Wa Alikiba Kwa Mwanaye Uliowapendeza Mashabiki Wengi

Ikiwa tayari ni siku chache zimepita, mtoto wa Staa wa muziki hapa nchini, Alikiba, Keyaan Alikiba alikuwa anasherehekea kumbukumbu ya kutimiza umri wa mwaka mmoja sasa jumatatu hii mkali huyo wa "Mbio", ametumia ukurasa wake wa Instagram, kupandisha picha mpya za Keyaan akiambatanisha na ujumbe mzuri kwa mwanae.
AliKiba ameandika, ''Mwaka wako wa kwanza ukawe mwanzo wa Miaka mingi iliyojawa upendo na furaha tele. Mwanangu Keyaan Alikiba KingKiba''

Aidha mkali huyo wa Bongo fleva ameonekana na mkewe wakiwa pamoja huku akiwa mwenye furaha kwenye hafla ya mtoto wao huyo wa kiume baada ya taarifa zilizoripotiwa mwishoni mwa mwaka jana kwamba ametengana na mkewe.


EmoticonEmoticon