Ulaya Yateswa Na Hali Mbaya Ya Hewa

Mvua kubwa na upepo mkali vimeikumba Uingereza na baadhi ya maeneo ya Ufaransa na kusababisha baadhi ya mashirika ya ndege kukatisha safari zake.

Huko Wales wakaazi walilazimika kuondoka kwenye makazi yao baada ya mvua kubwa kunyesha ndani ya kipindi cha masaa 48.

Uingereza imesambaza wanajeshi ili kukabiliana na athari za upepo mkali, mafuriko na maporomoko ya ardhi wakati kimbunga Dennis kikipiga England, Scotland na Wales siku ya Jumapili.

Rekodi 594 za tahadhari ya mafuriko zilitolewa kuanzia Scotland hadi England. Shirika la ndege la Uingereza British Airways na shirika la ndege la Easyjet yamethitibisha kusitisha safari zake za ndege.

Mtandao wa reli barani ulaya uliathirika na hali hiyo ya hewa jana jioni. Hali mbaya ya hewa pia imeiathiri Ufaransa na kutoa tahadhari ya mvua kubwa na mafuriko.


EmoticonEmoticon