Urusi Imejipanga Kwa Uchaguzi Wa Awamu Nyingine Ya Donald Trump.Je Imejipangaje?

Kitengo cha ujasusi cha Marekani kimeonya kwamba Urusi inajiribu tena kumsaidia rais Donald Trump kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Novemba kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini Marekani.
Matamshi hayo yanajiri baada ya mkutano wa faragha uliofanywa na kamati ya kijasusi mnamo tarehe 13 mwezi Februari , maafisa waliambia vyombo vya habari.
Rais Trump alidaiwa kukasirika , akilalama kwamba wanachama wa Democrats watatumia habari hiyo dhidi yake.
Alimbadilisha afisa mkuu wa ujususi Joseph Maguire siku ya Alhamisi. Gazeti la The New York Times liliripoti kwamba bwana Trump alikerwa kwamba Adam Schiff , mwanachama wa Democrat aliyeongoza kesi dhidi yake alikuwa katika mkutano huo.
Bwana Trump alishtakiwa na bunge la uwakilishi nchini Marekani kwa utumiaji mbaya wa mamlaka na kuzuia bunge la Congress. Aliondolewa makosa baada ya kesi hiyo iliochukua takriban wiki mbili katika bunge la seneti linalodhibitiwa na wanachama wengi wa Republican.
Wakati wa mkutano huo , wafuasi wa bwana Trump walihoji kwamba rais huyo alikuwa amechukuwa msimamo mkali , na kwamba ushirikiano wake na mataifa ya Ulaya umeimarishwa kutokana na hilo, lilisema gazeti hilo.
Bwana Schiff baadaye alituma ujumbe wa twitter kwamba iwapo bwana Trump alikuwa akiingilia kati ugawaji wa habari kati ya kitengo cha ujasusi cha Marekni na bunge la Congress kuhusu uingiliaji wa kigeni katika uchaguzi mkuu , rais alikuwa anahatarisha jaribio la kuzuia.


EmoticonEmoticon