Wananchi Waiomba Serikali Kuachana Na Swala La Kuwanyunyizia Nzige Dawa, Wawageuza Mboga

Wakazi wa Kaunti ya Bungoma ambayo ipo magharibi mwa taifa la Kenya ikiwa mpakani na Uganda wamejitokeza wakilalamika kuwa Nzige wamechelewa sana kuwafikia kwani wao huwatumia kama mboga.

Mbali na hilo pia wameiomba Serikali kuachana na suala la kuwapiga dawa kwani ni chakula chao labda wakapige dawa maeneo ambayo hawahitaji Nzige. Wakazi hao wameongeza kuwa Nzige kwani ni biashara na wanaamini uchumi katika eneo lao utakuwa sana kwa sababu watauza kama mboga sokoni.


EmoticonEmoticon