Waziri Mkuu Thomas Thabene Ashindwa Kufika Mahakani Kama Alivyoamriwa, Katibu Wake Atoa Sababu

Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane amekosa kufika mbele ya mahakama ambapo anakabiliwa na mashtaka ya kumuua mkewe wa zamani 2017.
Mshauri na mwana wa Thabane na mtoto wake anasema kwamba mzee huyo mwenye umri wa miaka 80 anapokea matibabu katika taifa jirani la Afrika kusini.
Mkewe wa sasa Maesaiah Thabane tayari ameshtakiwa na mauaji. Bwana Thabane atakuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kushtakiwa na mauaji akiwa afisini katika kesi iliolishanagaza taifa hilo dogo la Ufalme wa milimani.
Hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo. Maafisa wa polisi siku ya Alhamisi walisema kwamba atashtakiwa na mauaji siku ya Ijumaa. Alitarajiwa mahakamani mapema siku ya ijumaa, kulingana na ripoti za Reuters.
Hakwenda mahakamani , alienda Afrika kusini kwa matibabu , alisema katibu wake Thabo Thakalekoala akizungumza na chombo cha habari cha AFP, na kuongezea vilikuwa vipimo vya matibabu vya mara kwa mara.
Lakini naibu kamishna wa polisi Paseka Mokete aliambia waandishi habari kwamba alikuwa hajui kuhusu aliko bwana Thabane , lakini akasema kwamba iwapo angekuwa nje ya taifa akipokea matibabu basi wangelazimika kusubiri ili kuendelea na kesi atakapowasili.
'Hatuwezi kwa sasa kusema kwamba alikiuka agizo la mahakama''.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon