WHO Yatoa Takwimu Mpya Kuhusiana Na Virusi Vya Corona, Marekani Yaahidi Kutoa Msaada


Visa vya uogonjwa wa Coronavirus haviongezeki kwa kiwango cha juu nje ya China licha ya ongezeko la ugonjwa huo katika mkoa wa Hubei , kulingana na shirika la afya duniani.
Ongezeko la pekee ni lile la meli ya kitalii nchini Japan ambapo visa 44 vipya viliripotiwa na hivyobasi kuweka jumla ya walioambukizwa kuwa 218.
Pia imebainika kwamba hakuna mfumo wa jinsi watu wanavyoaga kulingana na WHO. Takwimu mpya kutoka katika mkoa wa Hubei sasa imefikia vifo 116 na visa 4,823.
Hilo ni ongezeko la chini ikilinganishwa na siku iliopita wakati kulipokuwa na ongezeko ambapo takriban vifo 240 viliripotiwa mbali na visa 15,000 vipya .
Hatahivyo visa vingi vinatoka Hubei ambapo watu wengi walipatikana na virusi hivyo hatari kulingana na Mike Ryan , mkuu wa mpango wa afya inayohohitaji dharura.
Hii haionyeshi mabadiliko makubwa kuhusu mtindo wa mlipuko huo alisema. Nje ya China kumekuwepo vifo viwili na visa 447 katika mataifa 24, alisema.
Siku ya Alhamisi Japan ilitangaza kifo chake cha kwanza cha virusi vya corona - ambaye alikuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 80 ambaye alikuwa akiishi Kanagawa kusini magharibi mwa mji mkuu wa Tokyo.
''Mwanamke huyo alipatikana na virusi hivyo baada ya kifo chake na kwamba hakuwa na uhusiano wowote na mkoa wa Hubei nchini China ambao ndio chanzo cha mlipuko wa corona''., vilisema vyombo vya habari vya Japan.
Siku ya alhamisi wizara ya maswala ya nchi za kigeni nchini Marekani ilisema kwamba ilikuwa ina wasiwasi kuhusiana na athari za mlipuko huo nchini Korea kaskazini, ambayo kufikia sasa haijaripoti kisa chochote.
Marekani imesema kwamba itatoa usaidizi katika taifa hilo kulingana na wizara hiyo.


EmoticonEmoticon