Boda Boda, Mabasi Madogo Na Makubwa Yapigwa Marufuku Uganda Kisa Corona

Rais museveni wa Uganda amepiga marufuku utumizi wa uchukuzi wa umma nchini Uganda
Katika hotuba yake kwa taifa Museveni alitangaza marufuku katika uchukuzi wote wa umma ikiwemo boda boda.
Mabasi madogo na yale makubwa yanayoelekea maeneo ya mashambani pamoja na magari moshi pia yamepigwa marufuku.
Magari ya kibinafsi yanaweza kutumika lakini sasa yatalazimika kubeba watu watatu pekee ikiwemo dereva.
Masoko nayo yatasalia wazi lakini yatakuwa yakiuza chakula pekee.
Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kuthibitisha visa vingine vitano vya ugonjwa wa coronavirus kikiwemo kisa cha mtoto mwenye umri wa miezi minane na hivyobasi kufanya visa hivyo katika taifa hilo kufikia idadi ya watu 14.
credit:bbc


EmoticonEmoticon