Cardi B Asema Mastaa Wanalipwa Kujitangaza Kuwa Wana Corona

Cardi B amesema kwamba anafikiri kuna mastaa wanalipwa pesa ili kujitangaza kuwa wana Corona.

Akiwa LIVE hapa IG, Cardi B alisema inakuaje kila aliyejitangaza amesema hakuwa na dalili sasa aliendaje kupima?

"Hebu tuseme kama ndio nina Corona sasa hivi. Nitajuaje kama nimepata kwa sababu muda mwingine nasikia 'Ukiwa na kikohozi basi umeambukizwa' Lakini nawaona hawa wacheza Kikapu wakisema 'Ndio nina Corona lakini sina dalili' Nyie watu mnacheza na mimi. Hilo ndio tatizo langu tu." alisema Cardi B.

Hadi sasa mastaa kama Tom Hanks na mkewe Rita Wilson wamejitangaza na wengine ni Idris Elba, Andy Cohen, Kevin Durant lakini wote walidai hawakuona dalili zozote.


EmoticonEmoticon