Davido Athibitisha Mpenzi Wake Kupata Maambukizi Ya Corona

Mchumba wa Davido, Chioma amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Amethibitisha Davido kwenye post yake kupitia account ya Twitter.
Amesema baada ya kurudi kutoka nchini Marekani ambapo alikatisha ziara yake, Mpenzi wake naye alirejea kutoka London alipokuwa na mtoto wao. Waliamua kupima pamoja, na Chioma aligundulika kuambukizwa virusi hivyo vya Corona. Jambo zuri ni kwamba mtoto wao (Ifeanyi) hajaambukizwa.

Kwa sasa Chioma amewekwa Karantini akiendelea kupokea matibabu huku Davido pia akijitenga kwa siku 14 kutazamia afya yake.


EmoticonEmoticon