Habari 5 Kubwa Za Soka Alhamisi March 19

1. Borussia Dortmund wamesonga mbele ya Liverpool, Manchester United na Chelsea katika kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na kiungo wa kati wa kikosi cha England cha vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 16, kutoka Birmingham msimu huu.

2. Manchester City, Juventus na Paris St-Germain wameonyesha nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mfaransa Houssem Aouar, mwenye umri wa miaka 21, kutoka klabu ya Ufaransa ya Lyon.

3. Chelsea wamezungumza na Barcelona kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba na kiungo wa kati Mbrazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo msimu ujao.

4. Arsenal wanasaini upya mkataba wa kumpoteza mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 30, msimu huu na wanataka garama ya euro milioni 55 (£50.7m) kwa ajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon ambaye anatafutwa Barcelona.

5. Manchester City na Manchester United wako tayari kumchukua kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, huku kijana huyo mwanye umri wa miaka 25- akihangaika kusaini mkataba mpya na Atletico Madrid.


EmoticonEmoticon