Habari 5 Kubwa Za Soka Ijumaa March 27

1. Chelsea, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich wote wamekuwa wakiwinda saini ya kiungo wa kimataifa wa vijana wa Espanyol Nico Melamed, 18, ambaye ana kifungu cha kutolewa cha pauni 7.3m.

2. Barcelona waitamani saini ya mchezaji wa ghali zaidi wa Tottenham Tanguy Ndombele, 23, ambaye alijiunga na timu hiyo ya kaskazini mwa London kwa pauni 55m kutoka Lyon msimu wa joto uliopita. 

3. Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo mwenye miaka 30, amepewa ofa ya kuongezewa mkataba wa miaka miwili na timu yake ya China Shanghai Shenhua huku mshahara ukipanda mpaka paundi 400,000 kwa wiki.

4. West Ham, Sporting Lisbon na Anderlecht ni kati ya vilabu vinavyo mtazama kipa wa Liverpool wa Ujerumani, Loris Karius, 26, ambaye yupo kwa mkopo Besiktas na anapatikana kwa pauni milioni 4.5 mwishoni mwa msimu.

5. Vilabu vya EFL vimeambiwa ligi haitarudi Aprili 30 na tarehe mpya ya kurejea kwa EFL itatangazwa wiki ijayo wakati mapambano dhidi ya kirusi corona yakiendelea


EmoticonEmoticon