Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne March 24

1. Beki wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 27, anatazamiwa kugoma kukataa ofa ya kujiunga na Manchester City mwishoni mwa msimu ili ajiunge na miamba ya Uhispania Real Madrid au Barcelona.

2. Klabu ya Chelsea inavutiwa kumsajili kiungo mkabaji wa West Ham na England Declan Rice, 21, katika dirisha la majira ya kiangazi. 

3. Manchester United wamepata anguvu mpya ya kumsajili kinda wa Birmingham Jude Bellingham, 16, baada ya Borussia Dortmund kufuta mipango yao ya kutaka kumsajili.

4. Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amekuwa akisaidia wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona kwa kuwapelekea chakula wazee karibu na uwanja wa mazoezi wa Spurs katika eneo la Enfield.

5. Mechi za Ligi ya Premia zinaweza kuchezwa nje ya jiji la London pale ligi itakapofunguliwa kwa kuwa jiji hilo lina idadi kubwa ya wagonjwa wa virusi cya corona.


EmoticonEmoticon