Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne March 31

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumanne Machi 31
1. Manchester United wameelekeza darubini yao kwa kiungo wa kati wa Leicester City na England James Maddison, 23, baada ya nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, ambaye wamekuwa wakimnyatia kwa muda mrefu kuhusishwa na kisa cha utata nje ya uwanja.
2. Real Madrid wanamfuatilia karibu nyota wa Sao Paulo Igor Gomes, 21, maarufu 'Kaka mpya' huku Barcelona, Sevilla na Ajax pia wakimng'ang'ania mchezaji huyo wa safu ya kati ya Brazili wa chini ya miaka 20.
3. Liverpool hawana mpango wa kumsajili tena kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ambaye yuko Bayern Munich kwa mkopo kutoka Barcelona.
4. Klabu za Arsenal, Tottenham na West Ham zinamnyatia beki wa Liverpool Dejan Lovren, 30, mkataba wake ukielekea ukingoni Anfield. 
5. Kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, amedokeza kuwa ataendelea kucheza katika Ligi Kuu ya soka ya England endapo ataondoka Stamford Bridge, hatua ambayo huenda ikafufua matumaini ya Arsenal na Tottenham kumsaka. 


EmoticonEmoticon