Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano March 18

1. Manchester City wametanga £80m kuwa bei ya kumuuza winga wa Algeria Riyad Mahrez, 29, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuenda Paris St-Germain.

2. Manchester United wanapanga 'mkakati' wa kusaini mkataba na beki wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, 26 msimu huu. 

3. Real Madrid wanapanga mikakati itakayomuwezesha mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30, kuondoka kwa uhamisho bila malipo.

4. Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumuuza kiungo wa kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 31, msimu wa joto huku wakiwa na mpango wa kubadili mkataba ake wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu.

5. Mmiliki wa Chelsea Mrusi Roman Abramovich, 53, ameripotiwa kushuka kwa thamani ya mali yake kwa hadi £2.4bn mwaka huu kutokana na mlipuko wa coronavirus japo thamani yake inakadiriwa kuwa zaidi ya £10bn.


EmoticonEmoticon