Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano March 25

1. Klabu za Liverpool, Manchester City na Arsenal zinavutiwa kumsajili beki kinda wa Schalke Malick Thiaw, 18, na mwenye urefu wa futi 6.3 ambaye mkataba wake umeweka Lima cha mauzo ya usajili cha pauni milioni 6.9.

2. Klabu ya Manchester United inaendelea kuamini kuwa kiungo nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 27, ataendelea kusalia Old Trafford huku wakitilia mashaka juu ya uwezo wa klabu yeyote kubwa Ulaya kumnunua.

3. Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 19, japo klabu za Manchester United na Tottenham pia zimeonesha nia ya kumsajili.

4. Winga wa Manchester City na England Raheem Sterling, 25, bado ana mapenzi na Liverpool licha ya kuondoka klabuni hapo kwa mazingira ya chuki. 
5. Wachezaji na wafanyakazi wa Juventus leo wanamaliza muda wao wa kujitenga na wataruhusiwa kutoka majumbani mwao.
Hata hivyo wachezaji watatu Daniele Rugani, Blaise Matuidi na Paolo Dybala watasalia karantini wakiendelea na matibabu ya virusi vya corona.


EmoticonEmoticon