Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatatu March 23

1. Klabu za Paris St-Germain, Real Madrid na Manchester City zote zinawania kumsajili beki wa Inter Milan na timu ya taifa ya Slovakia Milan Skriniar, 25.

2. Kusitishwa kwa soka ya ulaya kutokana na janga la corona kutaipatia Paris St-Germain nafasi wa kumshawishi shambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutia saini mkataba mpya japo mkataba wa sasa unaenedelea hadi 2022.

3. Barcelona wapo tayari kumuuza mshambuliaji wao Mfaransa are Antoine Griezmann, 29, kwa dau la Euro milioni 100 - ikiwa ni mwaka mmoja tu toka walipomsajili kwa dau la Euro milioni 120 akitokea klabu ya Atletico Madrid for 120m euros.

4. Liverpool na Arsenal walikuwa wanamfuatilia beki wa klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani Evan Ndicka, 20, kabla ya msimu kusimamishwa.

5. Barcelona wana nia ya kumsajili beki wa Manchester City na Ufaransa Aymeric Laporte, 25, katika majira ya kiangazi.

Wakati huo huo klabu hiyo wapo katika mazungumzo na wachezaji wao nyota ili kupunguza mishahara yao kutokana na klabu hiyo kuona kuwa haitaweza kuhimili bajeti ya mishahara inayofikia Euro bilioni 1 kwa kipindi cha msimu kilichobakia.


EmoticonEmoticon