Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatatu March 30

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumatatu Machi 30

1. Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal raia wa Gabon Emerick Aubameyang,30, endapo watashindwa kumpata Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund ama mchezaji wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane, 27 kutoka Liverpool.

2. Everton na West Ham wanafikiria kumsaini mshambuliaji wa Barcelona na Denmark Martin Braithwaite, 28, ijapokuwa klabu yake Barcelona haitamuuza kwa chini ya dau la £16m. Braithwaite alijiunga na Barca mwezi Februari katika usajili wa dharura.

3. Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, anafaa kuchukua fursa na kujiunga na Manchester United, kulingana na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Dimitar Berbatov.

4. Newcastle United wanapania kuwasajili kwa mkopo wachezaji wa safu ya kati ya Robbie Brady na Jeff Hendrick, walio na miaka 28. Mkataba wa wachezaji hao wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland katika uwanja wa Turf Moor unamalizika msimu huu wa joto.

5. Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan ana matumaini ya uhamisho wake wa mkopo kwenda Roma utageuzwa kuwa mkataba wa kudumu msimu huu . Arsenal wanataka £18m kumuachilia kiungo huyo wa miaka 31- raia wa Armenia, lakini klabu hiyo ya Italia inataka kulipa £10m tu.


EmoticonEmoticon