Idadi Ya Corona Uganda Yaongezeka Kwa Kasi

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) katika nchi za Afrika Mashariki za Uganda na Rwanda imepaa kwa kasi huku nchi hizo zikipambana kuzuia maambukizi zaidi.
Nchini Uganda jana usiku wametangaza wagonjwa wapya nane na kufikisha idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kufikia tisa.
Wagonjwa hao wapya wanane wote ni raia wa Uganda ambao wamerejea nchini humo kutokea Dubai baina ya tarehe 20 na 22 mwezi huu.
Waziri wa Afya wa Uganda, Jane Ruth Aceng amewaambia wanahabari kuwa kufikia sasa nchi hiyo imebaini wasafiri 2,661 wakiwemo raia wa nchi hiyo ambao wanaweza kuwa na hatari ya kusambaza maambukizi na watu wote hao wapo chini ya uangalizi maaalumu.

"Kati ya hao, watu 1,356 wanafuatiliwa kwa ukaribu; watu 774 wapo karantini kwenye maeneo maalumu yaliyotengwa huku 582 wakijitenga wenyewe kwa kujiweka karantini," ameeleza waziri Aceng.

Kwa mujibu wa waziri huyo wasafiri 1,305 tayari wameshamaliza kipindi cha siku 14 za kujitenga na kufuatiliwa hali zao.

Mgonjwa wa kwanza wa virusi hivyo anaelezwa kuendelea vizuri katika hospitali ya Entebbe.
credit:bbc


EmoticonEmoticon