Jimbo Kubwa Huko Marekani Limewaamuru Wananchi Wake Kukaa Nyumbani

Jimbo la California limewaamuru wakazi wake "kukaa nyumbani" huku likijaribu kudhibiti maambukizi ya coronavirus katika jimbo hilo maarufu zaidi nchini Marekani.
Govana Gavin Newsom aliwaambia wakazi wa California kuwa watatakiwa kuondoka majumbani mwao tu wakati ni muhimu wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.
Awali alikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 40 katika jimbo lake wanaweza kupata maambukizi ya virusi vya Covid-19 katika miezi miwili ijayo.
Virusi vya corona tayari vimewaua watu 205 nchini Marekani huku watu 14,000 wakipata maambukizi.
Kwa ujumla wagonjwa karibu 250,000 kote duniani wamepatikana na virusi hivyo vinavyosabisha ugonjwa kupumua na takriban 9,900 wamekufa.
Gavana Newsom alisema siku ya Alhamis jioni: "Wakati huu tunahitaji kuchukua maamuzi magumu.Tunahitaji kutambua hali halisi."
Amri yake itawaruhusu wakazi kuongoka majumbani mwao kununua mahitaji ya nyumbani au dawa, au pale wanapotembeza mbwa au wanapofanya mazoezi ya mwili, lakini itawataka kuacha mikusanyika ya watu.
Itawalazimisha biashara ambazo zinaonekana si za lazima kufungwa, huku ikiwaruusu wengine wanaofanya biashara za vyakula na mahitaji na bidhaa nyingine muhimu za nyumbani, maduka ya dawa, benki na vituo vya mafuta ya petroli kuendelea kufunguliwa.
Takriban nusu ya wakazi wa jimbo hilo wamekwishaanza kutekeleza hatua hizo kali, mkiwemo Jiji la San Francisco.


EmoticonEmoticon