Jumla Ya Wenye Corona Kenya Wafikia 42

Kulingana na waziri Kagwe visa vinne vilivyoongezeka vya COVID-19 vinalifanya taifa hilo kuwa na jumla ya visa 42, tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa tarehe 13 Machi.
Visa hivyo ni pamoja na Mkenya mmoja, raia mmoja wa Cameroon, Mmarekani mmoja na raia mmoja wa Burkina Faso . Akitoa taarifa kuhusu janga la coronavirus
Bwana Kagwe amewashauri Wakenya wote kushirikiana kuzuwia maambukizi ya corona badala ya kuuachia mzigo huo serikali pekee:'' Tunahitaji kufikiria jinsi ya kushughulikia tatizo hili kama serikali, jamii na kila mkenya'', amesisitiza Bwana Kagwe.
Amewaomba Wakenya kuwa tayari kwa hali yoyote inayoweza kujitokeza kutokana na virusi hivi na akasisitizia umuhimu wa waajiri kuwaruhusu wafanyakazi wao kuondoka kazini mapema kabla muda wa maruku ya kutotoka nje inayoanza saa moja jioni haijaanza kutekelezwa.
'Si haki kuwaachilia wafanyanyakazi muda wa kutotoka nje unakaribia, kama haitawezekana basi waajiri wawapatie malazi wafanyakazi wao'' amesema waziri Kagwe.


EmoticonEmoticon