Kauli Ya Donald Trump Yamtenganisha Chris Brown Na Familia Yake

Ugonjwa wa Corona wamtenganisha Chris Brown na familia yake, ashindwa kumuona mtoto wake wa Kiume AEKO

Mtandao wa HollywoodLife umeripoti kwamba baby mama wa Breezy, Ammika Harris alikwenda nchini Ujerumani pamoja na mwanae, sasa kufuatia tamko la Rais Trump juu ya kuzuia safari zote kwa nchi za Ulaya kuingia Marekani kutokana na Corona, hii imemfanya Chris Brown kuwa kwenye wakati mgumu wa kutomuona mwanaye huyo wa miezi 4.

Umoja wa Ulaya (EU) wametangaza kufunga mipaka yote ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Corona. 

Hii inazidi kumfanya mwimbaji huyo mwenye watoto wawili kutofahamu ni lini atamuona Aeko! Kikubwa anachokifanya kwa sasa ni kuwasiliana nao kwa njia ya mtandao tu, HL wameripoti kuwa Chris Brown ana FaceTimes na Ammika kila muda kuhakikisha wapo salama kiafya.


EmoticonEmoticon