Kiasi Cha Mabilioni Kilichotolewa Na Taasisi Ya Rihanna Kwaajili Ya Corona

Mwimbaji Rihanna kupitia taasisi yake iitwayo Clara Lionel Foundation yatoa kiasi cha ($5 Million) ambazo ni sawa na Bilioni 11.5 za Kitanzania kwa vikundi mbali mbali vya Afya na Mashirika kwa ajili ya kupambana na Virusi vya Corona nchini Marekani na maeneo mengine duniani kote.

Kwa mujubu wa mtandao wa TMZ fedha hizo zitatumika kuongeza nguvu ya kupambana na virusi vya Corona nchini Marekani na nchi nyinginezo kama vile Haiti na Malawi.

Hata hivyo chanzo kimeongeza kuwa dola 700,000 zitaenda moja kwa moja katika visiwa vya Barbados ambapo Rihanna amezaliwa.


EmoticonEmoticon