Kuna Uwezekano Wa Olimpiki Kuacha Kupeperusha Bendera Mwaka Huu Kisa Kikitajwa Kuwa Ni Corona

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) inaangalia uwezekano wa kuahirisha michuano ya Tokyo 2020, na imejipatia wiki nne kufanya maamuzi.
Bodi ya Utendaji ya IOC iliyokutana Jumapili jioni huku kukiwa na shinikizo kutoka kwa wanariadha na kamati za kitaifa za Olimpiki wakitaka michuano hiyo kusogezwa mbele kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
"Kutokana na hali kuwa mbaya duniani kote...bodi ya utendaji leo imeanzisha mchakato mpya wa mpango wa mazingira maalum," taarifa ya IOC imeeleza.
"Mazingira haya maalum yanahusiana na kuboresha mipango iliyokuwepo ya michezo kuanza Julai 24, 2020 lakini pia uwezekano wa kubadili tarehe ya kuanza kwa michezo."
Kuifuta kabisa "si moja ya ajenda" wamesema IOC lakini "kupunguza idadi ya michezo" kunaweza kufikiriwa pia.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe amekiri kwa mara ya kwanza kuwa  kuahirisha michuano ya Olimpiki ni jambo linalowezekana endapo hakutakuwa na uwezekano wa kuiandaa kwa "ukamilifu wake".


EmoticonEmoticon