Majimbo 50 Marekani Yakumbwa Na Mlipuko Wa Virusi Vya Corona, Gavana Atoa Kauli

Virusi vinavyoua vya coronavirus sasa vimekumba majimbo yote 50 huku jimbo la West Virginia likiripoti kisa cha kwanza cha maambukizi Jumanne.
Akitangaza kisa cha kwanza cha Covid-19 katika jimbo la West Virginia, Governor Jim amesema kuwa : "Tulifahamu kuwa hii inakuja."
Jiji la New York City limesema linaangalia uwezekano wa kufunga shughuli zote za umma sawa na ile iliyowekwa katika eneo la San Francisco Bay.
Kumekua na vifo 108 nchini Marekani vilivyotokana na coronavirus na zaidi ya visa 6,300 vimethibitishwa kote nchini Marekani.
Kumekua na takriban visa 200,000 kote duniani na karibu watu 8,000 wamekufa kutokana na virusi vya corona.
Huku utawala wa rais Trump ukiangalia jinsi ya kutoa pesa za kuchochea ukuaji wa uchumi zilizoripotiwa kuwa sawa na dola zipatazo bilioni $850, waziri wa fedha Steve Mnuchin akisema kuwa utawala "unaangalia jinsi ya kuwatumia hundi Wamarekani mara moja".
Kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia hadi 20% - kikiwa kimeongezeka mara dufu ikilinganishwa na wakati wa msukosuko mkubwa wa kiuchumi wa mwaka 2008.


EmoticonEmoticon