Marekani Ndyo Nchi Ya Kwanza Duniani Yenye Wagonjwa Wengi Wa Corona, China Ya Pili, Ikifwatiwa Na Italia

Marekani imethibishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani, kwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.
Kwa mujibu wa tawimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeipiku China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.
Lakini kukiwa na vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, na kuifanya Marekani ikiwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotoana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.
Idadi kubwa ya maambuizi imekujwa wakati ambao rais Donald Trump akitegemea kuwa hali itakuwa shwari muda si mrefu.


EmoticonEmoticon