Mashindano Ya Olimpiki Yaahirishwa Rasmi Kisa Corona

Waandalizi wa michezo ya Olimpiki Tokyo 2020, ambayo ilitarajiwa kung'oa nanga Julai 24, wamekubali kuahirisha michezo hiyo ya kimataifa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la coronavirus.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema kamati ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki imeafikiana kuhusu hatua hiyo baada ya kujipatia wiki nne kufanya maamuzi.
"Napendekeza tuahirishe michezo hii kwa mwaka mmoja, Rais wa [IOC] Thomas Bach kwa 100% ," alisema akikubaliana na ombi hilo.
Mashindano hayo bado yataitwa Tokyo 2020 licha ya kuwa itafanyika mwaka 2021.
Bodi ya Utendaji ya IOC iliyokutana Jumapili jioni huku kukiwa na shinikizo kutoka kwa wanariadha na kamati za kitaifa za Olimpiki wakitaka michuano hiyo kusogezwa mbele kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Katika taarifa ya pamoja, waandalizi wa Tokyo 2020 na IOC walisema:
"Kutokana na kasi ya mlipuko wa wa coronavirus hali kuwa mbaya duniani kote...bodi ya utendaji leo imeanzisha mchakato mpya wa mpango wa mazingira maalum," taarifa ilisema.


EmoticonEmoticon